Psalms 75

Mungu Ni Mwamuzi

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Zaburi ya Asafu. Wimbo.

1 aEe Mungu, tunakushukuru,
tunakushukuru wewe,
kwa kuwa jina lako li karibu;
watu husimulia matendo yako ya ajabu.

2 bUnasema, “Ninachagua wakati maalum;
ni mimi nihukumuye kwa haki.
3 cWakati dunia na watu wake wote inapotetemeka,
ni mimi ninayezishikilia nguzo zake imara.
4 dKwa wale wenye majivuno ninasema,
‘Msijisifu tena,’
kwa wale waovu, ‘Msiinue pembe zenu.
5 eMsiinue pembe zenu dhidi ya mbingu;
msiseme kwa shingo zilizonyooshwa.’ ”

6Hakuna yeyote atokaye mashariki wala magharibi
au kutoka jangwani awezaye kumkweza mwanadamu.
7 fBali Mungu ndiye ahukumuye:
Humshusha huyu na kumkweza mwingine.
8 gMkononi mwa Bwana kuna kikombe
kilichojaa mvinyo unaotoka povu
uliochanganywa na vikolezo;
huumimina, nao waovu wote wa dunia
hunywa mpaka tone la mwisho.

9 hBali mimi, nitatangaza hili milele;
nitaimba sifa kwa Mungu wa Yakobo.
10 iNitazikatilia mbali pembe za waovu wote,
bali pembe za wenye haki zitainuliwa juu.
Copyright information for SwhNEN